TANGAZO LA FURSA YA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI KUPITIA MRADI WA YEFFA

1. UTANGULIZI
Tanzania Agricultural Modernization Association (TAMA), kwa kushirikiana na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), inatekeleza Mradi wa  Ujasiriamali wa vijana kwa Mustakabali wa chakula na kilimo (Youth Entrepreneurship for the Future of Food and Agriculture -YEFFA), unaofadhiliwa na shirika la AGRA – Tanzania na kutekelezwa kupitia vyuo vya VETA.Manyara,Singida ,Dodoma na Tabora .
Mradi huu unalenga kuwajengea uwezo vijana 1,525 kwa kuwapatia ujuzi wa kiufundi na vitendo katika fani zifuatazo:

  • Ufundi wa Zana za Kilimo (Agro-Mechanization)- Mafunzo ni Mwezi mmoja
  • Umwagiliaji (Irrigation)-Mafunzo ni wiki mbili
  • Teknolojia ya Usimamizi wa Mazao Baada ya Mavuno (Post-Harvest Management Technology)- Mafunzo ni wiki mbili

TAMA, kwa kushirikiana na VETA, inakaribisha maombi ya kujiunga na Mafunzo ya Ufundi Stadi – Awamu ya Pili katika fani zilizotajwa hapo juu.
2. MIKOA ITAKAYONUFAIKA NA MAFUNZO
Mafunzo yatatolewa katika mikoa ya Manyara,Singida,Dodoma na Tabora
3. SIFA ZA KUJIUNGA
Mwombaji anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:
i. Awe Mtanzania mwenye umri wa miaka 18 hadi 35.
ii. Awe amehitimu elimu ya msingi au zaidi.
iii. Awe tayari kushiriki kikamilifu katika mafunzo kwa muda wote uliopangwa.
Wanawake na vijana wenye mahitaji maalumu wanahimizwa kuomba na watapewa kipaumbele.

 4. UTARATIBU WA KUOMBA
Maombi yanaweza kufanyika kwa njia zifuatazo:
i. Maombi ya mtandaoni (Online Application)
Kupitia kiunganishi (link) kitakachopatikana kwenye tovuti ya TAMA: www.tama.or.tz
ii. Maombi kwa nakala ngumu (Hardcopy):
Fomu zinapatikana katika maeneo yafuatayo:

  • Chuo cha VETA Manyara
  • Chuo cha VETA Singida
  • Ofisi ya Kata ya Gendabi – Manyara
  • Ofisi ya Kata ya Usagari – Tabora

Fomu zote za maombi zitatolewa bure.
5. KIPINDI CHA MAOMBI
Maombi yatafunguliwa kuanzia tarehe 12 Agosti 2026 na yatafungwa tarehe 23 Agosti 2026.
6. ADA NA GHARAMA ZA MAFUNZO
Gharama za ada ya mafunzo zitalipwa na Shirika la AGRA – Tanzania kupitia Mradi wa YEFFA.na gharama nyingine zinazohusiana na ushiriki wa mafunzo, ikiwemo nauli, chakula na malazi, zitalipwa na mzazi/mlezi au kijana mwenyewe.
7. MAWASILIANO
Kwa maelezo zaidi au ufafanuzi kuhusu mafunzo haya, wasiliana nasi kupitia:Simu: +255 664 378 334
                
                UFUNDI STADI, FURSA KAMA ZOTE